Connect with us

Makala

Azam Fc Yamsajili Chilambo

Klabu ya soka ya Azam Fc imefanikiwa kukamilisha usajili wa beki wa kulia wa klabu ya Ruvu Shooting Nathaniel Chilambo kwa mkataba wa miaka miwili ikiwapiku klabu ya Simba sc iliyokua inamnyemelea staa huyo kinda.

Azam Fc tayari wamemsainisha mkataba wa awali staa huyo ambaye alishakubaliana maslahi binafsi na klabu ya Simba sc ambapo alikubali dau la usajili kiasi cha shilingi milioni 30 za kitanzania na mshahara wa milioni 2 kwa mwezi ambapo amelazimika kusaini Azam Fc baada ya timu hiyo kumpa maslahi bora zaidi ya hayo.

Simba sc ilikua inahitaji beki wa kulia kumpa changamoto Shomari Kapombe huku katika ripoti za usajili jina la beki huyo lilikuwepo na sasa watalazimika kuangalia mbadala mwingine.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala