Connect with us

Makala

Azam Fc Yakomaa na Ibenge

Klabu ya Azam Fc imeanza mazungumzo na kocha wa klabu ya Al Hilal Fc Florent Ibenge ili kuinoa klabu hiyo kuchukua nafasi ya kocha Yousouph Dabo iliyemtimua wiki iliyopita.

Azam Fc inaamini Ibenge ni mtu sahihi kuchukua nafasi ya Dabo kutokana na kuwa na wasifu mzito akizifundisha klabu za As Vita,Rs Berkane na kufanikiwa kuzipatia mataji kadhaa makubwa barani Afrika.

Ibenge ambaye kwa sasa anaifundisha Al Hilal Fc ni kocha wa gharama kummliki ambapo mabosi wa Azam Fc wameamua kutojali kuhusu fedha wakitazama mafanikio zaidi kutokana na kuwa na mastaa wa gharama kikosini humo.

Azam Fc pia iliwahi kumtaka Nasredine Mohammed Nabi aliyekua kocha wa zamani wa Yanga sc lakini kocha huyo hakua tayari kuachana na klabu yake ya Kaizer Chiefs Fc ya nchini Afrika ya Kusini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala