Connect with us

Makala

Azam Fc Haitaki Utani Kabisa

Klabu ya Azam Fc imefanikiwa kumsajili kipa za zamani wa klabu ya Toulouse inayoshiriki ligi kuu nchini Ufaransa huku pia akichezea timu ya taifa ya Ufaransa chini ya miaka 20 Ali Ahmada ambaye pia ana uraia wa Comoro na Ufaransa.

Kipa huyo amesaini mkataba wa miaka miwili mbele ya mmiliki wa klabu hiyo Yussuph Bakhresa  pamoja na Afisa mtendaji mkuu wa klabu hiyo Abdulkarim Amin “Popat” kuja kuchukua nafasi ya kulinda lango la klabu hiyo ambayo ilikua imelegalega hasa msimu uliopita ambapo makipa Mathias Kigonya na Wilbol Maseke wameshindwa kuonyesha kiwango cha kuridhisha kiasi cha kufungwa mabao rahisi.

Ahmada mwenye miaka 30 ni Kipa mzoefu huku akiwa amecheza na mastaa wakubwa duniani wakina Gael Kakuta,akiwa sambamba na mastaa wengine Varane, Coquelin, Lacazette na wengineo.

mbali na kipa huyo klabu hiyo tayari imewanasa wazawa Abdul Sopu,Nathanael Chilambo,Cleophas Mkandala huku pia ikiwa imesajili wageni kama Issa Ndala,James Akaminko,Kipre Junior na Tape Edinho huku pia ikiwa imelifanyia mabadiliko makubwa benchi lake la ufundi kwa kuongeza kocha wa viungo,kocha wa washambuliaji na wengineo

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala