Connect with us

Makala

Man Utd Yaibomoa Ajax Fc

Klabu ya Manchester united imefikia makubaliano na Fc Ajax ya kumnunua beki Lisandro Martinez kwa dau linalotajwa kuwa kiasi cha paundi milioni 46 ambapo sasa mchezaji anakamilisha taratibu zingine ndogondogo za usajili ikiwemo kupimwa afya.

Usajili huo unaelekea kukamilika baada ya taarifa za muda mrefu kuhusu uwepo wa dili hili huku kikwazo kilikua ni makubaliano ya dau la usajili ambapo inasemekana mchezaji alikua tayari kwa uhamisho kwenda kuungana na kocha wake wa zamani Erick Ten Hag huku ilifikia hatua akitaka kugoma kufika mazoezini ili kulazimisha dili hilo.

Martinez ataungana na Ericksen ambaye tayari amekamilisha usajili kujiunga na timu hiyo huku akiwatosa vigogo kama Arsenal ambao nao walikua wanamnyemelea staa huyo mwenye uwezo wa kucheza kama beki wa kati na kushoto pamoja na kiungo mkabaji.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Makala