Connect with us

Makala

Ansu Fati apewa namba ya Messi Barca

Mshambuliaji kinda wa Fc Barcelona Ansu Fati ni kama amekabidhiwa mikoba ya gwiji wa timu hiyo Lionel Messi baada ya uongozi wa klabu hiyo kumkabidhi jezi namba 10.

Jezi namba 10 ilikuwa ikivaliwa na Messi aliyetimkia PSG majira haya ya joto baada ya mkataba wake kumalizika ndani ya Nou Camp na kushindwa kuingia mkataba mpya kutokana na sheria ngumu za la liga juu ya muundo wa mishahara.Messi alipewa jezi hiyo mwaka 2007 kutoka kwa Ronaldinho Gaucho.

Ansu mwenye miaka 18 ni zao la soka kutoka akademi ya Fc Barcelona ijulikanayo kama La Masia na alipandishwa kuitumikia timu ya wakubwa mwaka 2019 ambako alifanya vizuri na kuonesha kuwa atakuja kuwa mchezaji wa kutumainiwa ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake katika kitongoji cha Catalan.

Msimu wa 2020/2021 haukuwa mzuri kwa Fati baada ya kuumia na kukaa nje ya uwanja takribani msimu mzima na ndio kwanza amerejea kutoka majeruhi msimu huu.

Ansu Fati licha ya umri wake mdogo ameshaitumikia timu ya taifa ya Hispania na kupewa kwake jezi namba 10 ndani ya Barcelona ni imani kubwa ya Wakatalunya kuwa ataibeba timu hiyo kama alivyofanya mtangulizi wake japo ana viatu vikubwa sana vya kuvaa tokana na ubora mkubwa aliokuwa nao Lionel Messi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala