Connect with us

Soka

Morrison Amvaa Manara

Winga mwenye vituko wa klabu ya Simba sc Benard Morrison amemvaa msemaji wa klabu ya Yanga sc Haji Manara ambaye alikua anahamasisha mashabiki wa klabu ya Yanga sc kujitokeza kwa wingi uwanja wa ndege wa Jk Nyerere kumpokea staa Koffi Olomide anayewasili kuja kutumbuiza uwanja wa Taifa katika tamasha la wiki ya Mwananchi.

Morrison aliyekua anacheza Yanga sc kabla ya Simba sc kumsajili kimafia kiasi cha Yanga sc kukimbilia mahakama ya michezo ya kimataifa Cas kuhitaji ufumbuzi wa suala hilo,alimvaa Manara kupitia mtandao wa Instagram ambapo msemaji huyo alikua ameposti picha ikiwa na maneno kama inavyoonekana hapo chini.

Komenti hiyo ya Morrison imezua mtafaruku mitandaoni huku wadau wa soka nchini wakisubiri kuona manara atajibu nini maana inafahamika nae ni mtu wa vijembe.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka