Connect with us

Makala

Wydad Ac Yamsajili Mwalimu

Klabu ya soka ya Wydad Athletic Club imefanikiwa kuinasa saini ya mshambuliaji Selemani Mwalimu kutoka klabu ya Singida Black Stars baada ya kufikia makubaliano na timu hiyo kumsajili staa huyo mwenye mabao sita katika ligi kuu ya Nbc nchini.

Kocha Rulani Mokwena alikua na uhitaji mkubwa wa mshambuliaji wa kati ambapo alianza kumnyemelea mshambuliaji wa klabu ya Yanga sc Clement Mzize lakini baada ya dili hilo kushindikana aliamua kumsajili Mwalimu.

Tayari klabu yake ya Singida Black Stars imethibitisha kukamilika kwa dili hilo la mshambuliaji huyo aliyekua anaichezea Fountain Gate Fc kwa mkopo wa mwaka mmoja.

Mwalimu amesajili kwa dau linalokadiriwa kufikia kiasi cha shilingi milioni mia nane kwa mkataba wa miaka minne huku kukiwa na kipengele cha Singida Black Stars kupata asilimia kumi ya mauzo ya baadae.

Kwa upande wa maslahi binafsi pamoja na bonansi mbalimbali staa huyo pia atapokea mshahara wa milioni sita kwa mwezi katika mwaka wake wa kwanza wa mkataba huo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala