Connect with us

Makala

Uhamiaji Yathibitisha Mastaa Kubadili urai

Idara ya Uhamiaji ya Tanzania imethibitisha kuwa imewapa uraia wachezaji watatu wa timu ya Singida Black Stars baada ya wachezaji hao kuomba uraia kwa mujibu wa vifungu vya 9 na 23 vya sheria ya uraia ya Tanzania, Sura ya 357.

Wachezaji hao waliopewa uraia ni Emmanuel Keyekeh (Ghana), Josephat Arhur Bada (Cote d’Ivoire) na Muhamed Damaro Camara (Guinea) ambao kwa sasa wanahesabika kama raia wa Tanzania.

Taarifa ya Jana Januari 22, 2025 iliyotolewa na  timu hiyo ilithibitisha taarifa za wachezaji hao kuwa wamebadili uraia wa nchi zao na kuwa Watanzania.

Hata hivyo taarifa za ndani zinasema kuwa lengo kuu la mastaa hao kubadili uraia ni kuja kuwatumia katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania katika michuano ya Chan na Afcon ambayo itafanyika hapa nchini.

Mastaa hao wanadaiwa kuombwa Wizara ya Habari,Sanaa na Utamaduni nchini ili kupata wigo mpaka wa kikosi ili kufanya vizuri.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala