Connect with us

Makala

Baleke Kutua Afrika Kusini

Klabu ya Amazulu imeanza mazungumzo na TP Mazembe ili kuinasa saini ya mshambuliaji,Jean Baleke ambaye alikuwa akiitumikia klabu ya Yanga sc kwa mkopo wa mwaka mzima kabla ya mkataba huo kusitishwa.

Amazulu wamehamia kwa Baleke baada ya kuikosa saini ya Frank Ssebufu raia wa Uganda ambaye alikuwa akiitumikia New York Redbull II ya MLS.

Inaelezwa kuwa TP Mazembe wanahitaji angalau Dolan 80,000 ili kumuachia jumla Jean Baleke ambaye aliwahi kuitumikia klabu ya Simba Sc kwa misimu takribani miwili.

Baleke ameachwa na Yanga sc baada ya kocha Sead Ramovic kutoridhishwa na uwezo wake kutokana na kuonyesha kiwango cha kawaida uwanjani ambapo alifanikiwa kucheza michezo miwili pekee ya ligi kuu chini ya kocha aliyetimuliwa Miguel Gamondi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala