Connect with us

Makala

Mpole Ajiunga na Kagera Sugar

Nyota wa zamani wa klabu ya Geita Gold na FC Lupopo ya Dr Congo George Aman Mpole amejiunga na klabu ya Kagera Sugar baada ya kuachana na klabu ya Pamba aliyoitumikia kwa nusu msimu pekee.

Mpole hakuwa na wakati mzuri kwenye kikosi cha Pamba tangu aliposajiliwa kwenye dirisha kubwa msimu huu kama mchezaji huru baada ya kuachana na FC Lupopo ya DR Congo.

Tayari klabu ya Kagera Sugar imemtambulisha mchezaji huyo ambaye anachukua nafasi ya Obrey Chirwa ambaye amejiunga na Kengold Fc ya jijini Mbeya.

Mbali na Mpole klabu hiyo pia imekamilisha usajili wa kipa wa Klabu ya Simba Sc Ahmed Feruzi kwa mkopo wa nusu msimu sambamba na Shaphan Oyugi Siwa kutoka ligi ya Kenya.

Kagera sugar chini ya kocha Mellis Medo imeendelea na mazoezi makali kujiandaa na michezo ya ligi kuu nchini ambapo itaanza kucheza na Yanga sc mchezo wa kiporo mapema mwezi ujao.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala