Connect with us

Makala

Sowah Atua Singida Black Stars

Klabu ya Singida Black Stars imekamilisha usajili wa mshambuliaji raia wa Ghana Jonathan Sowah kwa mkataba wa miaka miwili kutoka klabu ya Al Nasser ya nchini Libya.

Usajili wa mshambuliaji huyo umekamilika baada ya tetesi za muda mrefu kuwa atajiunga na timu hiyo huku pia ikisemekana hata Yanga sc nao walikua wakimzea mate.

Singida Black Stars imemsajili mshambuliaji huyo baada ya kununua mkataba wake kutoka klabu hiyo na anatarajiwa kuungana na Elvis Rupia pamoja na Eliuter Mpepo kuongoza safu ya ushambuliaji klabuni hapo.

Ikiwa imemtambulisha kocha mpya Hamdi Miloud baada ya kuachana na kocha Patrick Aussems na benchi lake lote la ufundi,sasa klabu hiyo imeweka kambi maalumu ya mafunzo ambapo kocha huyo atachomeka mbinu zake kabla ya ligi kuu kurejea februari mosi.

Katika msimamo wa sasa wa ligi kuu nchini Singida ipo nafasi ya nne ikiwa na alama 33 baada ya kucheza 16 ya ligi kuu ya Nbc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala