Connect with us

Makala

Mwenda Mbioni Kutua Yanga sc

Klabu ya Yanga sc ipo mbioni kukamilisha usajili wa beki wa klabu Singida Black Stars Israel Mwenda kwa mkopo kuja kumpa changamoto beki Yao Kouasi Attouhoula sambamba na Nickson Kibabage.

Mabosi wa Yanga sc wameona usajili huo ni muhimu kutokana na majeraha ya mara kwa mara ya Yao Kouasi huku Kibwana Shomari akishindwa kumpa changamoto.

Mwenda aliyejiunga na Singida Black Stars akitokea Simba sc ambapo tangu asajiliwe mpaka sasa hajacheza hata mchezo mmoja wa ligi kuu nchini.

Usajili huo unaonekana kuwashangaza wengi huku wakihisi ni kama ilishapangwa tangu anaondoka Simba sc na safari ya Singida Black Stars ilikua kama geresha tu.

Mwenda pia anatajwa kuwa mbadala mzuri wa Chadrack Boka na Nickson Kibabage upande wa beki ya kushoto ambapo Boka amekua akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara.

Staa huyo tayari yupo jijini Dar es Salaam kukamilisha usajili huo ambapo mabosi wa Singida Black Stars wameshalizia ikisubiri kukamilika kwa maslahi binafsi baina ya klabu na mchezaji huyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala