Connect with us

Makala

Yanga sc Yaibamiza Jkt Tanzania

Ikitoka kushinda mchezo mgumu wa Kariakoo derby dhidi ya Simba Sc siku ya Jumamosi Oktoba 19,Klabu ya Yanga sc imeendeleza Ubabe katika ligi kuu ya soka ya Nbc nchini baada ya kuifunga Jkt Tanzania kwa mabao 2-0 katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam.

Kocha Mkuu wa Yanga sc Miguel Gamondi aliwapumzisha Stephan Aziz Ki,Khalid Aucho,Ibrahim Hamad Bacca,Chadrack Boka na Mudathir Yahaya huku akibadili muundo wa timu mpaka 3-5-2 ambapo Bakari Mwamnyeto aliungana na Dickson Job na Aziz Andambwile kuunga ukuta wa mabeki na Chama,Pacome na Mzize wakiongoza mashambulizi.

Iliwachukua Yanga sc dakika 23 kupata bao la kwanza likifungwa na Pacome Zouzoua aliyepokea pasi safi ya Cletous Chama na kuumalizia mpira uliomshinda kipa Dennis Richard.

Mwishoni mwa kipindi cha kwanza Denis Richard alifanya kosa na kudaka mpira uliopigwa na Pacome akiwa nje ya eneo la 18 na kupewa kadi nyekundu na mwamuzi Ahmed Arajiga ambapo pia alitoa faulo iliyopigwa kiufundi na Cletous Chama na kuiandikia Yanga sc bao la pili.

Jkt Tanzania waliamua kuepuka kipigo kikubwa kwa kuamua kupaki basi wakicheza nyuma zaidi ili kuizuia Yanga sc mpango ambao ulifanikiwa na mpaka dakika 90 zinatamatika Matokeo yalibaki hivyo hivyo.

Yanga sc imeendeleza wimbi la ushindi ikishinda michezo yote sita ya ligi kuu na kufikisha alama 18 ikiwa katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi huku Jkt Tanzania ikiwa imecheza michezo nane na kufikisha alama 10.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala