Connect with us

Makala

Tabora United Yavuna Alama 3 Namungo

Klabu ya Tabora United imeibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Namungo mchezo wa ligi kuu ya NBC uliochezwa leo Agosti 25,2024 katika uwanja wa Majaliwa ulioko wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.

Namungo ilitangulia kwa bao la kwanza lililofungwa na  Mcongomani Djuma SShabani kwa penati kabla ya Heritier Makambo kuchomoa pia kwa penati na dakika za mwishoni mwa mchezo alitoa pasi ya goli kwa Salum Chuku aliyefanikiwa kufunga bao la ushindi.

Huo ni mchezo wa pili kwa Tabora United msimu huu ambapo mchezo wa kwanza walifungwa 3-0 na Simba ilhali Namungo ni mchezo wa kwanza.

Tabora United baada ya kumaliza michezo ya ugenini sasa itacheza mechi zake tatu mfululizo katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi dhidi ya Kagera Sugar,Prisons na Fountain Gate.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala