Connect with us

Makala

Awesu Arudishwa Kmc

Shirikisho la Soka nchini Kupitia kamati ya usajili na hadhi za Wachezaji imeamuru mchezaji Awesu Awesu arejee katika klabu yake ya mwanzo ya Kmc badala ya Simba sc kutokana na usajili wake kutokua halali baada ya klabu ya Simba sc kutofuata utaratibu.

Awesu alijiunga na Simba sc baada ya kulipa kiasi cha shilingi milioni hamsini zilizoko katika kipengele cha mkataba wake endapo atataka kuondoka ambapo baada ya kulipa kiasi hicho alijiunga na Simba sc kwa mkataba wa miaka miwili.

Baada ya kutangazwa kujiunga na Simba Sc na kuelekea nchini Misri katika kambi ya maandalizi ya msimu klabu ya Kmc ilifungua shauri katika kamati hiyo ikidai kuwa kwa mujibu wa vipengele katika mkataba huo ilipaswa kuwe na mazungumzo baina ya pande mbili kabla ya kulipa kiasi hicho katika mkataba kama kinavyosema.

Kamati hiyo baada ya kupitia suala hilo hatimaye imeamuru kuwa usajili huo ni batili na mchezaji huyo anapaswa kurejea Kmc huku klabu ya Simba sc ikipewa onto kwa kutofuata utaratibu katika usajili huo.

Kwa upande wa mchezaji huyo amegoma kurejea klabuni humo akisema kuwa yuko tayari kuacha soka na si kurejea Kmc.

“Mimi saivi nipo njiani naenda mazoezini katika klabu ya Simba sc na niko radhi nistaafu kucheza mpira lakini sio kurejea katika klabu hiyo ya mwanzo” alisema Awesu akifanya mahojiano na chombo cha habari.

Pamoja na Shauri hilo pia klabu ya Simba sc msimu huu imeingia katika migogoro ya usajili ya wachezaji wengine watatu akiwemo Lameck Lawi,Yusuph Kagoma na Valentino Mashaka aliyekua Geita Gold Sc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala