Klabu ya Simba sc ikitoka nyuma kwa 1-0 imefanikiwa kushinda kwa mabao 4-1 katika mchezo wa ligi kuu ya soka ya Nbc dhidi ya klabu ya Geita Gold Sc uliofanyika katika uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam.
Ilimpasa kocha Juma Mgunda kufanya kazi ya ziada baada ya kutanguliwa kufungwa dakika ya Geofrey Julias dakika ya 11 ya mchezo kutokana na makosa binafsi ya kipa Hussein Abel ambaye hakua makini katika kuicheza krosi ya juu na mpira kumponyoka na kumkuta mfungaji.
Uwepo Saido Ntibanzokiza,Fabrice Ngoma,Ladack Chasambi na Mzamiru Yassin ulikua nguzo imara kwa Simba sc kutokana na kazi kubwa waliyoifanya katikakati mwa kiwanja na kuwalazimu Geita Gold Sc muda mwingi kubaki nyuma wakitegemea mashambulizi ya kushtukiza.
Dakika za nyongeza kuelekea mapumziko Saido Ntibanzokiza alifunga kwa penati na kuifanya mchezo uwe 1-1 baada ya Shomari Kapombe kuangushwa eneo la hatari na mwamuzi kuamuru pigo hilo.
Kipindi cha pili hasa dakika za mwishoni zilikua chungu kwa Geita Gold Sc kwa walishushiwa mvua ya mabao kupitia kwa Saido Ntibanzokiza kwa faulo dakika ya 72 huku Ladack Chasambi akifunga mabao mawili dakika za 86 na 90+3 na kupeleka msiba Geita.
Simba sc sasa imefikisha alama 63 katika nafasi ya tatu ya msimamo ikizidiwa wastani wa magoli ya kufunga na kufungwa na Azam Fc iliyokatika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi kuu nchini baada ya michezo 28 ya ligi kuu huku Geita Gold sc mpaka sasa ikiwa katika nafasi ya 15 akiwa na alama 25 katika michezo 28.