Connect with us

Soka

Fainali Crdb Yahamishiwa Zanzibar

Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) sasa limeamua kuuhamishia mchezo wa fainali wa michuano ya kombe la Shirikisho la Crdb baina ya Yanga sc na Azam Fc katika uwanja wa Amaan mjini Unguja kutoka ule wa awali wa Tanzanite ulioko mkoani Manyara.

Taarifa iliyotolewa na Shirikisho hilo imesema kuwa imeamua kuchuakua uamuzi huo baada ya kujiridhisha kuwa uwanja wa Tanzanite hauko tayari kutokana na kutokamilika kwa baadhi ya maandalizi muhimu ikiwemo majukwaa na miundombinu mingine.

Mchezo huo kufanyika visiwani humo umepongezwa na wadau wa michezo nchini kutokana na ukweli kwamba uwanja huo una miundombinu mizuri huku pia idadi ya mashabiki watakaoenda viwanjani kushuhudia mchezo huo itakua kubwa ukichagizwa na uwepo wa wachezaji wenye asili ya huko kama Feisal Salum,Mudathir Yahaya na Ibrahim Hamad Bacca.

Yanga sc na Azam Fc zinatarajiwa kumenyana June 2 katika uwanja huo ambapo mchezo huo utakua mkali kutokana na ubora wa timu zote mbili huku Azam Fc ikihitaji kurudisha kisasi cha kufungwa 1-0 katika fainali iliyopita mkoani Tanga.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka