Mchezo ujao wa Ligi Kuu baina ya Klabu ya Simba sc dhidi ya JKT Tanzania FC utapigwa Alhamisi Februari 15, 2024 saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo ulioko eneo maarufu la Mbweni jijini Dar es salaam.
Mchezo huo wa kufunga dimba kwa duru la kwanza la ligi kuu ya Nbc nchini kwa timu hizo utafanyika uwanjani hapo baada ya Shirikisho la soka nchini kuruhusu matumizi ya uwanja huo wa jeshi kwa michezo ya ligi kuu ukiwa kama uwanja wa nyumbani wa timu ya Jkt Tanzania.
Simba sc mpaka sasa ina alama 33 katika michezo 14 katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi kuu ambapo itakua na nia ya kuchukua alama tatu ilikufikisha 35 ambazo zitapunguza pengo la alama dhidi ya Yanga sc mwenye alama 40 kileleni mwa msimamo huku pia alama hizo zitaofanya klabu hiyo kuizidi Azam Fc kwa alama nne zaidi.
Endapo Jkt Tanzania itapata alama tatu katika mchezo huo basi itasogea mpaka nafasi ya nane ya msimamo ambapo itafikisha alama 19 kutoka 16 za sasa katika nafasi ya 14 ya msimamo.
“Haitakuwa mechi rahisi, tunawajua JKT ni timu nzuri lakini tumejipanga na tutaingia kwenye mchezo wa kesho kwa lengo la kutafuta pointi tatu.” Alisema Nahodha Msaidizi, Mohamed Hussein.
“Tunahitaji kuufungue vyema uwanja wetu wa nyumbani dhidi ya Simba SC” Kocha Msaidizi wa JKT Tanzania, George Mketo alisema wakati akieleza utayari na malengo yao katika mchezo wa kesho dhidi ya Simba SC kwenye NBC Premier League.