Connect with us

Makala

CR7 Bado Yupo Sana

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno na klabu ya Al Nassr Cristiano Ronaldo ameiambia klabu yake kuwa kabla hajaenda kujiunga na timu yake ya taifa anataka kuongeza mkataba mpya mpaka mwaka 2027.

Cristiano Ronaldo mipango yake ni kwamba mpaka mkataba huo utakapoisha basi atatangaza rasmi kustaafu soka kwani pia anampango wa kucheza kombe la dunia la mwaka 2026 hivyo baada ya hapo atacheza msimu mmoja akiwa na Al Nassr halafu atastaafu soka.

Mpaka sasa pamoja na kwamba ametimiza umri wa miaka 38 bado staa huyo ana nguvu za kucheza kushinda hata vijana wa miaka 24 huku hilo likichagizwa na bidii yake ya mazoezi na kujitunza huku akiwa hatumii kabisa vilevyi vya aina yeyote ile.

Ronaldo amefanikiwa kuwa staa maarufu zaidi duniani ambapo amefanikiwa kucheza vilabu vikubwa kama Manchester United,Real Madrid,Juventus,Sporting Lisbon alikoanzia soka mpaka sasa amehamia Uarabuni.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala