Connect with us

Makala

Sakho Atwaa Tuzo CAF

Mshambuliaji wa klabu ya Simba sc Pape Osman Sakho amefanikiwa kutwa tuzo ya goli bora barani Afrika katika michuano ya klabu bingwa ambapo amepata tuzo hiyo inayotolewa na shirikisho la soka barani Afrika (Caf) usiku wa kuamkia leo.

Katika kipengele hicho Sakho alikua anachuana na staa wa Orlando Pirates ya Afrika ya kusini Gabadinho Mhango ambaye alifunga goli katika michuano ya mataifa ya Afrika (Afcon) dhidi ya Morroco pamoja na staa wa Morroco Zouhair El Mautaraj ambapo bao la Sakho dhidi ya Asec Mimosa ndilo ambalo lilishinda tuzo hiyo katika usiku uliokua na mastaa wengi waliohudhuria akiwemo Jay Jay Okocha,Sadio Mane,Samuel Etoo na wengineo.

Sakho ndo anakua mchezaji wa kwanza anyecheza ligi kuu kutwaa tuzo hiyo tangu ianzishwe huku baada ya kutwaa tuzo hiyo baadhi ya timu kubwa barani Afrika na ulaya tayari zimeanza mchakato wa kutaka kuvunja mkataba wake katika klabu ya Simba sc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala