Connect with us

Makala

Yanga sc,Morrison Wamalizana

Taarifa za kuaminika kutoka kwenye vyanzo mbalimbali zinasema kuwa, klabu ya Dar Young Africans imemalizana na nyota wake wa zamani raia wa Ghana, Bernard Morrison kwa ajili ya kupata huduma yake kwenye msimu ujao katika michuano mbalimbali.

Morrison ambaye hivi karibuni alitangazwa kupewa likizo ya hadi mwisho wa msimu na klabu yake ya Simba na taarifa za sasa kuripoti kuwa amemalizana na klabu ya Yanga huenda akawepo kama mtazamaji kwenye mchezo wa Nusu Fainali ya FA inayotarajiwa kuzikutanisha timu za Simba na Yanga ndani ya dimba la CCM Kirumba Mwanza.

Mpaka sasa licha ya kupewa mapumziko ya muda usiojulikana na klabu yake ya Simba sc lakini mchezaji huyo mpaka sasa bado hajasafiri kuelekea nchini Ghana ambapo inasemekana yupo nchini huku akiwa hapokei simu za waajiri wake klabu ya Simba sc na tayari ameanza mazungumzo ya kurudi Yanga sc klabu ambayo ilimleta hapa nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala