Connect with us

Makala

Dtb Wamvizia Wawa

Klabu ya Dtb iliyopanda kucheza ligi kuu msimu ujao inaangalia uwezekano wa kumsajii beki wa klabu ya Simba sc Serge Paschal Wawa endapo klabu hiyo itaaamua kutomuongezea mkataba mpya baada ya mkataba wa sasa kuelekea ukingoni.

Klabu hiyo inayodhaminiwa na benki ya Dtb inaamini kuwa uzoefu wa beki huyo ni kitu muhimu sana kwa maendeleo ya klabu hiyo kunako michuano ya ligi kuu nchini huku akiwa na uzoefu wa kukutana na washambuliaji hatari wa ligi kuu na wale wa kimataifa.

Wawa anamaliza mkataba wake na klabu ya Simba sc ambayo mpaka sasa haijaonyesha nia ya kumsainisha mkataba mpya baada ya kutua klabuni hapo misimu mitatu nyuma akitokea nchini Sudan.

Uwepo wa Joash Onyango na Henock Inonga ndio sababu kuu ya Wawa kukosa nafasi kikosini humu ambapo mara nyingi hukaa benchi ama kucheza michezo michache endapo mmoja katika mabeki hao anapokosekana.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala