Connect with us

Makala

Pablo Kusalia Simba sc

Uongozi wa klabu ya Simba sc umeamua kwa pamoja kusalia na kocha Pablo Franco pamoja na kutotimiza masharti aliyopewa kwenye mkataba wake ya kuhakikisha kuwa klabu hiyo inatwaa makombe yote na kufika hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la shirikisho ama klabu bingwa barani Afrika.

Kocha huyo raia wa Hispania amebahatika kusalia klabuni hapo baada ya kufanikiwa kuifikisha klabu hiyo hatua ya robo fainali ya kombe la shirikisho huku pia kitendo cha kutolewa kwa matuta na Orlando Pirates huku wakishinda mchezo wa kwanza jijini Dar es salaam kikimbeba kiasi cha kuwashawishi viongozi kumuongezea muda zaidi huku wakimpa mamlaka yote ya usajili wa mastaa wa kikosi hicho msimu ujao huku akichagua wachezaji wa kuwatema.

Pablo aliikuta Simba sc ikiwa imetolewa na Jwaneng Galaxy Fc katika kombe la klabu bingwa barani Afrika na kusababisha kocha Didier Gomez kutimuliwa klabuni hapo na kuletwa Pablo kuchukua nafasi yake ambapo alikuta tayari mastaa wakiwa wamesajiliwa tayari huku yeye akiwa na kazi ya kuwatengeneza.

Inasemekana pamoja na kubakishwa klabuni hapo kocha huyo ana kazi ya kuhakikisha Simba sc inatwaa taji la tano mfululizo la ligi kuu mbele ya Yanga sc anayeongoza ligi akiwa na alama 53 huku Simba sc akiwa na alama 40 na mchezo mmoja mkononi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala