Connect with us

Makala

Kabudi Akutana na Viongozi TFF,Yanga Sc na Simba Sc

Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mh.Palamagamba Kabudi amekutana na viongozi wa klabu za Simba sc na Yanga pamoja na wale wa Shirikisho la soka nchini sambamba na Bodi ya Ligi kuu ili kumaliza mgogoro uliotokea machi 8 na kusababisha mchezo baina ya timu hizo kutofanyika.

Kabudi alikutana na viongozi wa pande hizo ili kusikia na kisha kujua aanzie wapi kutatua suala hilo la klabu hizo kugomea mchezo huo na kusababisha taswira ya soka nchini kuchafuka.

Mkutano huo ulifanyika katika ofisi ya Baraza la michezo nchini (Bmt) zilizopo katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mbali na Waziri Kabudi pia Naibu Waziri Mh.Hamis Mwinjuma sambamba na Katibu mkuu wa Wizara hiyo Mh.Gerson Msigwa walihudhuria kikao hicho ambacho kila upande ulifanya kikao kwa muda wake.

Akizungumza baada ya kikao hicho Rais wa klabu ya Yanga sc Eng.Hersi Said alisema kuwa mkutano huo umekua na faida kwao kama klabu.

“Mheshimiwa waziri alikuwa na mwanzo mzuri kwa kusema kuwa kikao chao sio sehemu inayoweza kutoa maamuzi ila ni kikao cha kutafuta njia ya utatuzi kwa tatizo lililotokea ila alitaka kujua kutoka Yanga nini kinawatatiza”,Alisema Hersi

Pia kwa upande wa Simba sc Mwenyekiti wa klabu hiyo Mh.Murtaza Mangungu alisema kuwa wao wamezungumzia kuhusu maendelea ya soka nchini.

“Sisi Simba tumeitwa kujadili kuhusu soka la Tanzania na maendeleo yake na Waziri, hatujaitwa hapa kujadili kuhusu mchezo wetu dhidi ya Yanga na kama ingekuwa hivyo tungeitwa wote kwa pamoja, wao kama wamejadili kuhusu mchezo huo ni wao sasa ila sisi hatujajadili hilo kwanza hata sifahamu kama Yanga walikuwepo”,Alisema Murtaza Ally Mangungu, Mwenyekiti wa klabu ya Simba Sc.

Mpaka sasa bado haijajulikana kuhusu mstakabali wa mchezo huo lakini mpaka sasa inaonekana Wizara inatamani mgogoro huo umalizike kwa amani.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala