Connect with us

Tenis

Raducanu atwaa US Open

Mchezaji kinda wa mchezo wa tenisi kutoka Uingereza Emma Raducanu amefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano mikubwa ya mchezo huo(Grandslam) ya US Open baada ya kumtwanga kinda mwingine Leylah Fernandez kutoka Canada kwa upande wa wanawake.

Raducano mwenye miaka 18 amemfunga Fernandez(19) kwa seti 6-4,6-3 katika mechi bora ya fainali na kuvunja ukame wa miaka 44 kwa Uingereza kutioshinda grandslam yoyote upande wa wanawake kwa mchezaji mmoja mmoja tangu afanye hivyo Virginia Wade aliyefanya hivyo mara ya mwisho mwaka 1977 aliposhinda michuano ya Wimbledon.

Virginia Wade alikuwepo pia uwanjani hapo kumshuhudia Raducanu akitwaa ubingwa huo mkubwa duniani na alionesha kuwa na hisia za furaha baada ya kumshuhudia kinda huyo akivunja rekodi hiyo.

Emma Raducanu amefanya maajabu makubwa na anakuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya mchezo huo kushinda grandslam akianzia michezo ya awali ya mtoano kutokana kuwa katika viwango vya chini vya ubora vya mchezo huo akiwa namba 150.

Mchezaji huyo amepokea salamu za pongezi kutoka kwa watu maarufu duniani akiwemo malkia wa Uingereza Elizabeth.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Tenis