Connect with us

Tenis

Tenisi:Australia yamzuia tena Djokovic

Serikali ya Australia imeifuta tena VISA ya mchezaji namba moja duniani kwa ubora upande wa wanaume kwenye mchezo wa tenisi Novak Djokovik raia wa Serbia.

Maamuzi hayo yamefanya na Waziri wa Uhamiaji wa nchi hiyoAlex Hawke yakiashiria kuwa mchezaji huyo anapaswa kuondoka kndani ya nchi hiyo haraka ikiwa ni kusimamia kanuni zao za kiafya na hadhi ya Taifa hilo licha ya kuwa na ratiba ya kucheza siku ya Jumatatu kwenye michuano mikubwa duniani ya Australian open.

Mshindi huyo mara tisa wa michuano hiyo alikuwa na kibarua cha kutetea ubingwa huo kuanzia wiki ijayo na kufukuzia rekondi ya kutwaa taji la 21 la Grand slam litakolomfanya kuwa mwana tenisi wa kiume mwenye maanikio zaidi duniani akiwapiku Roger Federer na Rafael Nadal ambao amefungana nao kwa kuwa na mataji makubwa 20 kila mmoja.

Hapo awali Djokovic alifutiwa VISA yake kwa kushindwa kuthibitisha kuwa hastahili kupewa chanjo baada ya kuingia nchini humo kinyume na sheria,japo mahakama kuu nchini humo iliufuta uamuzi huo wa serikali lakini mamlaka ya nchi hiyo yamezuia tena asishiriki michuano hiyo.

Hata hivyo bado nyota huyo ana nafasi ya kukata tena rufaa kuhakikisha anasalia Australia na kutetea ubingwa wake kwa upande wa wanaume.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Tenis

  • Medvedev ashinda US Open

    Mchezaji wa tenisi wa Russia Daniil Medvedev amefanikiwa kutwaa ubingwa wa US Open upande...

  • Raducanu atwaa US Open

    Mchezaji kinda wa mchezo wa tenisi kutoka Uingereza Emma Raducanu amefanikiwa kutwaa ubingwa wa...