Connect with us

Tenis

Medvedev ashinda US Open

Mchezaji wa tenisi wa Russia Daniil Medvedev amefanikiwa kutwaa ubingwa wa US Open upande wa wanaume baada ya kumfunga mchezaji namba moja wa tenisi upande wa wanaume Novak Djokovic kwa seti 6-4,6-4,6-4 kwenye mchezo wa fainali uliofanyika usikuwa kuamkia leo.

Djokovic tayari alikua ameshinda grandslam tatu za Australian Open,Fresh Open pamoja na Wimbledon na alikua katika nafasi ya kuwa mchezaji wa sita kwenye historia ya mchezo huo kushinda grandslam zote kubwa tatu ndani ya mwaka kabla ya Medvedev kuzuia hilo.

Medvedev alionekana kumtawala zaidi mpinzani wake ambaye alionekana kutokuwa vizuri kimwili.

Huo unakuwa ushindi wa kwanza kwa Medvedev na mchezaji kutoka Russia kushinda grandslam baada ya miaka mingi.Mrusi huyo sio mtu wa mchezo mchezo kwani anashikilia namba mbili katika mchezo huo upande wa wanaume.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Tenis