Connect with us

Makala

Yanga Sc Yazindukia Ruangwa

Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kupata ushindi baada ya kuukosa katika michezo yake miwili iliyopita ya ligi kuu ya Nbc nchini baada ya kuifunga Namungo Fc kwa mabao 2-0 katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Majaliwa Complex wilayani Ruangwa.

Yanga sc ikicheza mchezo wa kwanza wa ligi kuu ikiwa na kocha mpya Sead Ramovic iliibuka na ushindi huo kwa mabao ya kipindi cha pili ambapo Kennedy Musonda alipokea pasi nzuri ya Maxi Nzengeli na kumchungulia kipa Benno Kakolanya kwa shuti kali na kuibua shangwe kwa mashabiki waliojaa uwanjani hapo.

Mabadiliko ya kumuingiza Cletous Chama na kumtoa Stephan Aziz Ki yalizaa matunda kwa Yanga sc baada ya staa huyo kutoa pasi safi ya bao kwa Pacome Zouzoua dakika ya 67 na kuihakikishia ushindi Yanga sc.

Katika mchezo huo Kipa Abubakar Khomeini alikua na mchezo mzuri baada ya kuziba vilivyo pengo la Djigui Diarra huku pia kiungo Duke Abuya akicheza vizuri eneo la kiungo cha ulinzi akiziba nafasi ya Khalid Aucho ambaye ni majeruhi kiasi cha kupewa tuzo cha mchezaji bora wa mchezo huo.

Kutokana na ushindi huo sasa Yanga sc imefikisha alama 27 nyuma ya Simba Sc iliyokileleni na alama 28 huku timu zote zikicheza jumla ya michezo 11 ya ligi kuu ya Nbc nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala