Connect with us

Soka

Yanga Sc Yawasili Afrika Kusini

Msafara wa wachezaji,Mashabiki na viongozi wa klabu ya Simba sc umewasili salama nchini Afrika kusini tayari kwa mchezo wa marudiano wa hatua ya robo fainali dhidi ya Mamelod Sundowns ya nchini Afrika ya kusini utakaofanyika jijini Pretoria siku ya ijumaa saa tatu usiku.

Kikosi hicho mapema kiliwasili katika uwanja wa Oliver Tambo jijini Johanesburg kisha kusafiri kwa barabara kuelekea jijini Pretoria ambapo basi la kusafiria la wachezaji liliharibiki kilomita tano kutoka uwanja wa ndege na kuwalazimu wachezaji kupanda basi dogo lililokua linatumiwa na waandishi wa habari pamoja na viongozi ili kuwahi kwenda kupumzika hotelini na wengine kutafuta basi jingine kwa msaada wa ubalozi wa Tanzania nchini humo.

Sambamba na msafara huo pia msafara mwingine ambao umegharamiwa na serikali unatarajiwa kuwasili nchini humo siku ya Alhamis ambao utafika kwa usafiri wa basi ambao walianza safari siku ya Jumatatu mchana tayari kuwahi mchezo huo sambamba na kuongeza nguvu ya ushangiliaji.

Tayari kikosi hicho kimefanya mazoezi kwa mara ya kwanza usiku ya kuamkia April 3 ambapo kesho kinatarajiwa kufanya mazoezi katika uwanja wa Loftus Versfeld ambao ndio uwanja wa nyumbani wa Mamelod Sundowns Fc ambao pia hutumika kwa michezo ya rugby.

Yanga sc inahitaji sare yeyote ya mabao ama ushindi wa aina yeyote ili kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo tangu ianzishwe mwaka 1935.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka