Connect with us

Soka

Yanga sc Yamnyatia Beki Angola

Inaripotiwa kuwa Mabosi wa Yanga wameanza kumnyatia beki wa kushoto wa kimataifa wa DR Congo, Lomalisa Mutambala anayecheza soka la kulipwa nchini Angola katika timu ya Sagrada Esperanca aliyokua anaichezea Carlos Calinhosi ambaye alikua kiungo mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo.

Klabu hiyo itakua na nafasi nzuri ya kumsajili beki huyo ikizingatiwa  kuna uhusiano mzuri kati ya vigogo wa Yanga na Sagrada baada ya awali kukamilisha dili la Carlinhos kuja Jangwani japo hakua na maisha mazuri klabuni hapo.

Beki huyo anakuja kuongeza nguvu upande wa kushoto ambako imemlazimu kocha Nasredine Nabi kumhamishia Kibwana Shomari baada ya Yassin Mustapha na David Bryson kushindwa kuonyesha makali eneo hilo huku majeraha ya mara kwa mara yakisababisha viwango vyao kutokua imara.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka