Connect with us

Makala

Yanga Sc Yaikota Alama Tatu Kmc

Licha ya kuendelea kutopata ushindi wa mabao mengi kama inavyotarajiwa na wengi bado klabu ya Yanga sc imeendelea kuokota alama kwenye michezo yake ya ligi kuu baada ya kushinda kwa 1-0 dhidi ya Klabu ya Kmc katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika katika uwanja wa Chamazi Complex uliopo jijini Dar es Salaam.

Yanga sc ikianza mchezo na mastaa wake takribani wote wakiongozwa na Cletous Chama na Stephan Aziz Ki ilishambulia kwa kasi dakika za mwanzoni mwa mchezo na kufanikiwa kupata bao la mapema dakika ya 5 ya mchezo kupitia kwa Max Nzengeli baada ya mabeki na kipa wa Kmc kujichanganya kuokoa mpira uliopigwa na Yao Kouasi Attouhoula.

Kmc walicheza kwa mbinu kubwa wakiwasubiri Yanga sc golini kwao huku wakishambulia kwa kushtukiza mpango ambao uliwaweka salama katika dakika zote za mchezo huo.

Yanga sc haikua na kiwango chake cha kawaida wakikubali kupiga pasi nyingi eneo lao na juu ya msitari lakini walishindwa kupata bao licha ya kujaa mastaa hodari kwa kutupia akiwemo Prince Dube ambaye pia alimpisha Jean Baleke.

Mpaka dakika tisini za mchezo huo zinatamatika Matokeo talibaki 1-0 na kuifanya Yanga sc kufikisha alama tisa ikishinda michezo yote mitatu ya ligi kuu iliyocheza mpaka sasa huku Kmc ikifikisha alama tano ikicheza michezo sita ya ligi kuu ikiwa katika nafasi ya kumi na moja ya msimamo wa ligi hiyo ya sita kwa ubora barani Afrika.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala