Connect with us

Soka

Yanga Sc Yaachana na Moloko,Konkoni

Klabu ya Yanga sc imeamua kuachana na mastaa wake wawili jesus Moloko na Hafidh Konkoni kutokana na kocha Miguel Gamondi kutoridhishwa na viwango vyao katika kikosi hicho kinachowania ubingwa wa ligi kuu nchini kwa mara ya tatu mfululizo.

Yanga sc imeamua kuachana na Moloko kwa makubaliano ya pande mbili baada ya mchezaji huyo kubakiza mkataba wa miezi sita huku kocha Miguel Gamondi akionyesha kutomhitaji kikosini na Konkoni yeye ametolewa kwa mkopo katika klabu ya Dogan Tûrk Birligi ya Cyprus mpaka mwishoni mwa msimu huu.

Yanga sc kuziba nafasi hizo imewasajili Augustine Okrah sambamba na Joseph Guédé Gnadou ambao wataingizwa kwenye usajili wa Yanga sc na kutimiza idadi ya wachezaji 12 na kigeni ambao wanatakiwa kwa mujibu wa kanuni za bodi ya ligi kuu nchini.

Yanga sc katika msimamo wa ligi kuu nchini ipo nafasi ya pili ikiwa na alama 31 ikiwa imecheza jumla ya michezo 11 ambapo Azam Fc ipo kileleni mwa msimamo ikiwa na alama 33.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka