Connect with us

Soka

Yanga sc Watua Arusha Kibabe

Kikosi cha mabingwa wa Ligi Kuu Bara 2023/2024, Yanga kimewasili jijini Arusha leo na kitacheza mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) dhidi ya Ihefu Mei 19, 2024 kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta, kuanzia saa 9:30 Alasiri.

Katika msafara wa klabu hiyo mastaa kama Khalid Aucho,Kennedy Musonda na wengine walionekana wakishuka katika ndege akiwemo Augustine Okrah ambaye hakucheza michezo kadhaa kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

Yanga sc inatarajiwa kukutana na upinzani mkali mbele ya Ihefu Fc yenye mastaa wa maana wa kimataifa huku pia ikiwa na kiu ya kutwaa taji la kwanza kubwa nchini tangu ianzishwe ili ipate nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa mwakani.

Mara kadhaa Yanga sc imekua ikipoteza michezo ya ugenini dhidi ya klabu hiyo japo mara ya mwisho iliiadhibu kwa mabao 5-1 katika mchezo wa ligi kuu katika uwanja wa Chamazi jijini Dar es salam.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka