Baada ya kuinyuka Coastal Union 1-0 katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc uliofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta jijini Arusha,Klabu ya Yanga sc leo imeanza safari ya kuelekea Zanzibar kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Singida Black Stars.
Mchezo baina ya miamba hiyo unatarajiwa kufanyika Visiwani humo katika uwanja wa New Amaan Complex siku ya Oktoba 30.
Black Stars wenyewe tayari wameshawasili Visiwani humo kwa ajili ya mchezo huo ambao wao ni wenyeji ambapo kikakuni wanaruhusuliwa kucheza michezo miwili ne ya uwanja wao wa nyumbani wa Ccm Liti ambao upo kwenye matengenezo.
Yanga sc wanakabiliwa na ratiba ya michezo mitatu migumu ambapo walianzia ugenini dhidi ya Coastal Union na sasa wanakwenda Zanzibar kwa ajili ya mechi hiyo dhidi ya Singida Black Stars inayonolewa na kocha wa zamani wa klabu ya Simba Sc Patrick Aussems ambayo mpaka sasa haijafungwa mchezo wowote kwenye ligi kuu wakiwa kileleni mwa msimamo na alama 19.
Wakimaliza mchezo huo Yanga sc watarudi katika uwanja wa Chamazi Complex kuvaana na Azam Fc ambayo nayo ni timu ngumu kufungika hasa inapocheza na Yanga sc ambapo mchezo huo huwa wa kukamiana sana.
Endapo kocha Miguel Gamondi atafanikiwa kuchukua alama tatu katika kila mchezo dhidi ya timu hizo basi itakua ishara nzuri kwake kuwa mastaa wa kikosi hicho wapo tayari kwa ubingwa wa ligi kuu ya Nbc kwa mara nyingine tena na wakiwa tayari wametwaa taji la ngao ya jamii.