Connect with us

Makala

Yanga sc Kuwakosa Aucho,Mzize

Kikosi cha Yanga Sc kitaendelea kuwakosa wachezaji wake Khalid Aucho, Clement Mzize ambao ni majeruhi huku Ibrahim Bacca naye akikosekana kutokana na kutumikia adhabu ya kadi nyekundu.

Msafara wa Yanga sc tayari leo umewasili Ruangwa,Lindi kwa ajili ya mchezo dhidi ya Namungo FC utakaofanyika siku ya Jumamosi, Novemba 30 katika uwanja wa Majaliwa mkoani humo.

Ikiwa imetoka kupoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya Al Hilal Fc katika mchezo wa klabu bingwa barani Afrika huku pia ikiwa haijapata ushindi katika michezo yake miwili ya ligi kuu ya Nbc,Yangavsc itahitaji alama tatu ili kurejea kwenye ubora wake.

Aucho na Mzize ni wachezaji muhimu klabuni hapo kutokana na ubora wao ambapo kocha Sead Ramovic anaweza kuwatumia Jonas Mkude na Kennedy Musonda katika nafasi hizo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala