Connect with us

Makala

Yanga Sc Kukipiga na Kaizer Chiefs

Klabu ya Yanga sc inatarajiwa kushiriki michuano maalumu ya Toyota yaliyoandaliwa na klabu ya Kaizer Chiefs ya nchini Afrika ya kusini siku ya Julai 28 mwaka huu nchini humo ikiwa ni moja ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu na michuano ya kimataifa.

Yanga sc inatarajiwa kuweka kambi ya maandalizi hayo nchini humo kwa msimu huu ambapo tayari mastaa wa kikosi hicho tayari wameshaanza kuingia kambini Avic Town na muda wowote kuanzia sasa wanatarajiwa kusafiri kuelekea nchini Afrika ya kusini kwa ajili ya maandalizi hayo.

 

Rais wa klabu hiyo Eng.Hersi Ally Said tayari amehudhuria ufunguzi wa michuano huyo nchini humo siku ya Julai 8 mbele ya viongozi wa klabu hiyo sambamba na wadhamini wa michuano hiyo kampuni ya Toyota.

“Mchezo huu unaendeleza uhusiano kati ya timu zetu kubwa mbili barani Afrika ambao ulianza mwaka jana tulipowaalika Kaizer Chiefs kushiriki katika Tamasha la Wiki ya Mwananchi. Tunafurahia mwaliko huu na tunaahidi kutoa mchezo wa ushindani utakaotusaidia kujiandaa kwa msimu mpya wa 2024/25.”Alisema Hersi akizungumza na vyombo vya habari nchini humo.

Kikosi cha Kaizer Chiefs tayari kimeingia kambini nchini Uturuki kujiandaa na michuano hiyo huku Yanga sc ikiingia kambini Avic Town tayari kwa ajili ya michuano hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala