Connect with us

Makala

Yanga Hii Usipime Kabisa

Ndivyo wanavyosema mashabiki na wapenzi wa klabu ya Yanga sc baada ya kuishuhudia klabu hiyo ikipambana na timu ya Augsburg fc katika mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu katika maandalizi ya msimu ujao.

Yanga sc ambayo kwa sasa ipo nchini Afrika kusini imefanikiwa kucheza mchezo huo na timu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Ujerumani baada ya kupata nafasi ya kushiriki michuano ya Mpumalanga Cup inayofanyika nchini humo ikishirikisha pia timu za Augsburg Fc ya Ujerumani,Mbabana Swalows ya Botswana na Ts Galaxy ya Afrika ya kusini.

Augsburg ambayo msimu uliopita ilimaliza nafasi ya kumi na moja katika ligi ya Ujerumani maarufa kama Bundesliga ikusanya alama 39 ilifanikiwa kulinda mabao yake mawili dhidi ya Yanga sc na mchezo huo kumalizika kwa 2-1 huku mabao ya Augsburg yakifungwa na Mads Pedersen dakika ya 27 na Philipe Tietz dakika ya 80 huku Yanga sc wakipata bao la kufutia machozi dakika ya 86 kupitia kichwa safi cha Jean Baleke aliyefunga akiunganisha krosi ya Maxi Nzengeli.

Uimara wa kipa Djigui Diarra ndio ulisaidia kuwaweka mchezoni Yanga sc kutokana na kuokoa nafasi nyingi zilizoonekana kuwa magoli ya wazi kabisa huku uwepo wa Stephan Aziz Ki na Cletous Chama uliwapa wakati mgumu wapinzani kutokana na maarifa ya ziada ya wachezaji hao japo bado wanaonekana hawajaelewana sana.

Yanga sc ambayo imesheheni mastaa wa kila aina iliamua kuwaanzisha benchi Prince Dube,Jean Baleke,Aziz Andambilwe na Duke Abuya ambao wamesajiliwa msimu na walipoingia kipindi cha pili walionyesha kiu ya kutaka kuanza kikosi cha kwanza.

Katika mchezo huo mastaa Kennedy Musonda na Khalid Aucho walianzia jukwaani huku Pacome Zouzoua akishindwa kuungana na timu kutokana na kuwa na ruhusa maalumu ya kushughulikia hati ya kusafiria ambayo imemlazimu kurudi nchini kwao Ivory Coast.

Yanga sc bado ipo nchini humo ikiendelea na maandalizi ya msimu ambapo wikiendi hii ya Julai 27 itacheza na Kaizer Chiefs katika mfululizo wa michezo yake ya maandalizi ya msimu wa 2024/2025 na inatarajiwa kurejea nchini mwanzoni mwa mwezi August kwa ajili ya kilele cha Tamasha la wiki ya Mwananchi itakayofanyika August 4 katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala