Connect with us

Soka

Try Again Awapiga Biti Mastaa Simba sc

Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya klabu ya Simba sc Salum Abdalah maarufu kama “Try Again”amewapiga biti zito mastaa wa timu hiyo ikiwa zimebaki siku takribani tisini ili dirisha dogo la usajili lifunguliwe hapa nchini.

Bosi huyo mnene klabuni hapo amewataka mastaa hao kukaza buti kwani hakutakua na simile katika kuchukua hatua hasa kwa wale ambao watashindwa kuushawishi uongozi wa klabu hiyo kutokana na viwango vyao.

Try Again amesema hayo leo Jumanne, Novemba 14, 2023 baada ya kuulizwa mpango wao wa usajili dirisha dogo ambapo amekiri kuwa wataachana na wachezaji wote ambao wameshindwa kuipambania timu.

“Tuna mwezi mmoja na nusu kabla ya dirisha dogo la usajili ni muda wachezaji kupambania nafasi hiyo kujihakikishia nafasi ya kubaki, kwani hatutakuwa na sababu ya kubaki na wakaa benchi ambao wanalipwa hela nzuri na hawaipambanii timu;

“Wakati tuna pambana na matokeo mazuri kiwanjani tunatakiwa kuwa na wachezaji wapambanaji kama Kibu Denis ambaye kwasasa amekuwa muhimu kikosini akitoka tu unaona timu ikiyumba.” alisema.

Katika kipindi hiki kilichosalia kuelea usajili wa dirisha dogo mastaa hao hawana budi kuonyesha viwango katika michuano ya kimataifa ambayo Simba sc itafungua dimba dhidi ya Asec Mimosa siku ya Novemba 24 katika hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka