Connect with us

Makala

Tabora United Yakana Chikola Kujiunga na Kmc

Timu ya Tabora United imekana kuhusu kuachana na mshambuliaji wake Offen Chikola ambaye ameripotiwa kujiunga na Klabu ya Kmc Fc yenye makazi yake jijini Dar es Salaam.

Taarifa za awali zilieleza kuwa klabu ya Kmc imekamilisha usajili wa Chikola kutoka Tabora United kuchukua nafasi ya kiungo mshambuliaji wake Ibrahim Elias ambaye hayupo katika kambi ya timu hiyo mpaka sasa.

Taarifa iliyotolewa na uongozi wa Klabu hiyo umesema kuwa mchezaji huyo ana mkataba na klabu hiyo mpaka mwisho wa msimu huu hivyo hajaondoka klabuni hapo.

Msimu huu Chikola amekua msaada mkubwa klabuni hapo akiungana na Heritier Makambo na Yacouba Sogne kuunda safu hatari ya ushambuliaji iliyoifikisha timu hiyo katika nafasi ya tano ya msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala