Connect with us

Soka

Stars Yaichapa Mongolia

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo wa kirafiki wa Fifa Series dhidi ya Mongolia uliofanyika nchini Azerbaijan na kukamilisha ratiba ya michezo hiyo ya kirafiki iliyochini ya kalenda ya Fifa.

Aali Stars katika mchezo wa awali ilikubali kipigo cha 1-0 kutoka kwa Bulgaria katika mchezo wa kwanza nchini humo na hatimaye leo imefanikiwa kuibuka na alama tatu muhimu ambazo zitaisaidia kuongeza alama katika viwango vya ubora wa soka vya Fifa.

Katika mchezo huo mabao ya Taifa Stars yalifungwa na Kelvin John dakika ya 49 huku Abdul Sopu akifunga bao la pili dakika ya 62 kwa shuti la mbali baada ya kuchungulia kipa Mongolia huku Novatus Dismas akimalizia kalamu ya ushindi kwa Taifa Stars akifunga bao la tatu dakika ya 76 ya mchezo.

Kikosi hicho kikiwa chini ya kocha Hemed Morocco kinatarajiwa kuanza safari ya kurejea nchini kesho mapema ambapo siku ya Jumatano kinatarajiwa kuwasili na kutoa nafasi kwa wachezaji wa klabu za Simba sc na Yanga sc ambao bado hawajajiunga na timu hizo kuungana na timu zao kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya michezo ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka