Connect with us

Soka

Simba sc Yaweka Mzigo Kwa Mwamnyeto

Klabu ya Simba sc imewasiliana na meneja wa beki wa klabu ya Yanga sc Bakari Mwamnyeto ili kuweza kumsajili baada ya mkataba wake na klabu ya Yanga sc kuelekea mwishoni ambapo utafikia tamati agosti mwaka huu.

Meneja wa beki huyo anaitwa Kassa Mussa anayeishi nchini Italia kwa sasa tayari amepokea ofa hiyo nono ya klabu ya Simba sc ikitaka kumsajili beki huyo ili akawe mbadala wa beki Serge Pascal Wawa ambaye viongozi wa klabu hiyo wamekubaliana kuachana nae wakiona kuwa umri umemtupa mkono huku beki Joash Onyando nae akiwa hajasaini mkataba mpya mpaka sasa.

Pia licha ya klabu ya Simba sc kuweka ofa hiyo mezani pia ipo klabu ya kutoka nchini Uturuki ambayo pia imeonyesha nia ya kumsajili beki huyo kijana na nahodha wa klabu ya Yanga sc ambayo nayo imeonyesha nia ya kuendelea kuwa nae ikitaka kuongeza mkataba nae huku pia mchezaji mwenyewe akiwapa kipaumbele wanajangwani hao.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka