Connect with us

Makala

Simba Sc Yasajili Straika la Mabao

Klabu ya Simba sc imekamilisha usajili wa mshambuliaji raia wa Uganda Stephen Mukwala kwa mkataba wa miaka miwili akiwa huru baada ya kumaliza Mkataba na klabu yake ya mwanzo ya Asante Katoko ya nchini Ghana.

Mshambuliaji huyo yupo kwenye kiwango bora sana hasa msimu uliopita ambapo amepata nafasi katika kikosi cha timu ya Taifa ya Uganda katika kuwania kufuzu michuano ya kombe la Dunia ambapo amefunga jumla ya mabao mawili mpaka sasa.

Simba sc imelazimika kufanya kazi ya ziada kumshawishi staa huyo kutua klabuni humo kutokana na kuwa na ofa za ulama ambazo inasemekana kuwa alizikataa.

Mshambuliaji huyo anafuata nyayo za mastaa wengine wa Ugands waliowahi kusajiliwa na klabu hiyo wakiwemo Emmanuel Okwi,Juuko Murshid,George Owino na wengineo ambao baadhi leo wameacha alama klabuni hapo hasa Okwi.

Mukwala Ana kazi rahisi sana kuwania namba mbele ya Pa omar Jobe na Fredy Michael ambao bado hawajawashawishi mabosi wa timu hiyo mpaka sasa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala