Connect with us

Soka

Simba sc Yajibu Shutuma za Orlando

Kufuatia kufungwa 1-0 na klabu ya Simba sc katika mchezo dhidi ya Orlando Pirates ambapo Kocha wa Klabu hiyo Mandla Ncikazi aliituhumu klabu ya Simba sc kwa kutumia mbinu chafu nje ya uwanja.

Ncikazi alitoa shutuma hizo baada ya mchezo huo ambapo aliishutumu klabu hiyo kuhusu mapokezi mabovu pamoja na kutotumika kwa Var (Video Assistance Reffaree) uwanjani hapo hali iliyosababisha klabu ya Simba sc ipate penati ambayo ilitokana na Benard Morrison kuangushwa eneo la 18 huku wachezaji wa Orlando wakimtaka mwamuzi kujiridhisha kwa Var.

Tukio hilo lilileta mijadala mbalimbali barani Afrika hasa nchini Tanzania na Afrika ya kusini huku kocha huyo akisema kuwa Simba sc wamebebwa na leo hii klabu ya Simba sc imejibu shutuma hizo kwa kutoa tamko rasmi kwa waaandishi wa habari kama linavyosomeka hapo chini.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka