Connect with us

Makala

Simba Sc Yaingia 2025 Kileleni

Baada ya kupata ushindi wa 1-0 katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini dhidi ya Klabu ya Singida Black Stars sasa rasmi klabu ya Simba Sc itaingia mwaka 2025 ikiwa katika kilele cha msimamo wa ligi kuu nchini.

Simba sc ilipata alama tatu katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Ccm Liti mjini Singida shukran kwa bao pekee la Fabrice Ngoma aliyeunganisha kona safi ya Jean Charles Ahoua dakika ya 42 ya mchezo huo uliokua mkali na wa kusisimua kutokana na ushindani baina ya timu hizo.

Singida Black Stars inabidi wajilaumu wenyewe kutokana na kupoteza muda mwingi kumlalamikia mwamuzi badala ya kucheza mpira hali iliyochangia kuwatoa mchezoni mara kwa mara.

Kipa Moussa Camara alionyesha umahiri wake mara kadhaa akicheza mipira ya hatari kutoka kwa Elvis Rupia aliyekua hatari katika mchezo huo.

Mpaka dakika tisini zinamalizika katika mchezo huo Simba sc ilichukua alama tatu na kufikisha alama 41 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yeyote katika kipindi hiki cha raundi ya 15 ya ligi kuu nchini.

Sasa ligi kuu inakwenda katika mapumziko ya wiki mbili ili kupisha michuano ya kombe la Mapinduzi ambalo linashirikisha timu za Taifa inayotarajiwa kuanza Januari 3 mwaka 2025.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala