Connect with us

Soka

Simba Sc Yafungwa na Wajelajela

Klabu ya Simba sc imekubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Tanzania Prisons Fc katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro ikiwa ni mchezo wa raundi ya 16 wa klabu hiyo.

Uamuzi wa Mwalimu Abdelhack Benchika kuwapumzisha Mohamed Hussein,Ayoub Lakred,Che Fondoh Malone ulimtokea puani baada ya Samson Mbangula kufunga mabao mawili katika mchezo huo dakika za 45+3 na 62 ambapo aliwachomoka mabeki wa Simba sc kwa bao la kwanza na kumfunga kipa Aishi Manula ambaye hakupiga hesabu zake vizuri huku akiwapiga chenga Henock Inonga na Kennedy Juma la kufunga bao la pili.

Simba sc walikua wanajisahau mara kwa mara na kwenda kushambulia ambapo mabeki wa klabu hiyo walikua wanakabia juu ya mstari wa katikati na kusababisha hatari pindi wanaposhambuliwa.

Kuingia kwa Saido Ntibanzokiza na Ladack Chasambi kuliwapa uhai Simba sc na kufanikiwa kufanya mashambulizi makali langoni mwa Prisons huku kipa Yona Amosi akifanya kazi ya ziada kuokoa hatari langoni lakini alishindwa kuzuia shuti la Fabrice Ngoma dakika ya 89 na kuruhusu bao kwa Simba sc.

Pamoja na jitihada za Simba sc kusaka bao la kusawazisha lakini uimara wa mabeki Tanzania Prisons wakiongozwa na Nurdin Chona uliwasaidia wageni kuchukua alama tatu na kufikisha alama 27 katika nafasi ya tano ya msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini.

Simba sc sasa rasmi imezidiwa alama saba na wapinzani wake Yanga sc wenye alama 43 wakiwa na michezo sawa huku Azam Fc mwenye michezo ishirini mpaka sasa akiwa na alama 44 katika ligi kuu nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka