Connect with us

Makala

Simba Sc Yafanya Balaa Mbeya

Klabu ya Simba Sc imeanza kurejesha furaha kwa mashabiki zake baada ya kukusanya alama tatu katika mchezo mgumu wa ligi kuu ya Nbc nchini dhidi ya Tanzania Prisons uliofanyika katika uwanja wa sokoine Jijini Mbeya.

Ikitoka kufungwa 1-0 na Yanga sc siku ya Jumamosi Oktoba 19 na kupoteza alama tatu,Simba sc ilipaswa kushinda mchezo huo ili kurejesha imani kwa mashabiki wake.

Kocha Fadlu Davis alipumzisha baadhi ya mastaa kama Jean Charles Ahoua,Abdulrazak Hamza,Yusuph Kagoma sambamba na Joshua Mutale kutokana na majeraha waliyoyapata katika mchezo wa derby.

Simba sc ilipata bao pekee la mchezo huo dakika ya 5 likifungwa na Che Malone Fondoh aliyeunganisha mpira uliotemwa vibaya na kipa wa Tanzania Prisons Mussa Mbisa na kumkuta mfungaji.

Bao hilo lilidumu mpaka dakika 90 za mchezo huo ambapo pamoja na kuwa na mpira wa kushambuliana kwa zamu hakuna timu ambayo ilifanikiwa kupata bao.

Simba sc sasa imefikisha alama 16 ikicheza michezo saba ya ligi kuu ya Nbc nchini huku Tanzania Prisons ikiwa imecheza michezo 8 ikivuna alama 7 pekee.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala