Connect with us

Makala

Simba Day Kiboko

Tamasha la klabu ya Simba sc maarufu kama Simba day limefanyika kwa mafanikio makubwa ikiwa ni mara ya 16 ambapo limefanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam siku August 3.

Mgeni rasmi katika Tamasha hilo alikua Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mh.Hamad Masauni aliyesindikizwa na Naibu Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.Hamis Mwinjuma sambamba na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh.Albert Chalamila.

Mashabiki wa klabu hiyo walijitokeza kwa wingi kuanzia asubuhi wakipanga mistari kwenye milango ya uwanja kuingia uwanjani huku burudani mbalimbali zikipamba ndani ya uwanja.

Timu ya wanawake wa klabu hiyo ilianza kuingia uwanjani majira ya saa saba mchana kupambana na Mlandizi Queens ambapo Simba queen iliibuka na ushindi wa mabao 7-0.

Msanii Alikiba aliyekua mtumbuizaji mkuu alifanikiwa kukonga nyoyo za mashabiki wa klabu hiyo baada ya kushusha burudani ya maana akisaidiwa na madensa wakiongozwa na Angel Nyigu.

Baada ya utambulisho wa wachezaji uliofanywa na meneja wa habari wa klabu hiyo Ahmed Ally ndipo ulipotimu wasaa wa mastaa wa klabu kuonyesha uwezo dhidi ya kikosi cha Apr Fc ya Rwanda.

Kocha Fadlu Davis aliamua kuanza na Ali Salim,Shomari Kapombe,Mohammed Hussein na Che Malone akisaidia na Chamou Karabou eneo la ulinzi wa kati na kiungo kikiwa na Mzamiru Yassin,Fabrice Ngoma huku Joshua Mutale,Awesu,Ahoua na Mukwala wakiongoza safu ya ushambuliaji.

Kikosi hicho kiliteseka na muunganiko kutokana na wachezaji kutofahamiana vizuri huku kipindi cha pili yakifanyika mabadiliko makubwa wakiingia Deborah Fernandes na Augustine Okejepha ambao walifanya kazi kubwa kubadili mchezo.

Deborah alifunga bao la uongozi kwa shuti kali mapema kipindi cha pili huku Edwin Balua alipiga faulo iliyozaa bao la pili dakika za mwishoni mwa mchezo.

Mpaka mchezo unakamilika Simba sc ilimaliza na ushindi wa 2-0 dhidi ya Apr Fc na kuhitimisha tamasha hilo la 16 ya Simba day.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala