Connect with us

Makala

Sillah Awekwa Mtu Kati Azam Fc

Klabu ya Azam Fc imempa ofa ya mwisho kiungo mshambuliaji wake Gibril Sillah ili asaini mkataba wa miaka miwili klabuni hapo ama achukue uamuzi mwingine huku klabu hiyo ikitafuta mbadala wake.

Iko hivi,Sillah aliyesajiliwa miaka miwili iliyopita kutoka Raja Casablanca mkataba wake unatarajiwa kufika tamati mwishoni mwa msimu huu na baada ya majadiliano kutofikia muafaka klabu hiyo imempa ofa ya dola 125,000 ili asaini ndani ya siku saba na kama ikishindikana basi itajiandaa na kuanza kutafuta mbadala wake.

Mshambuliaji huyo raia wa Gambia amekua na mchango mkubwa klabuni hapo na mpaka sasa pamoja na ofa ya klabu yake hiyo inasemekana tayari ana ofa ya klabu ya Yanga sc pamoja na klabu nyingine mbili za nje ya Tanzania.

Yanga sc wanaangalia uwezekano wa kumsajili Sillah kutokana na kocha Sead Ramovic kuhitaji Mshambuliaji wa pembeni ama winga mwenye kasi ili kuongeza mashambulizi kutokea pembeni.

Upande wa menejimenti ya mchezaji huyo mpaka sasa bado haijatoa jibu lolote kuhusu ofa hiyo ya mwisho ya klabu ya Azam Fc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala