Connect with us

Soka

Samatta Agombewa Ulaya

Timu za Brighton na Aston Villa zinashoriki ligi kuu ya Uingereza zimeonesha nia ya kumuwania mshambualiaji wa kitanzania anayecheza ligi kuu nchini Ubeligiji Mbwana Samatta ili akajiunge na timu hizo kwa ajili ya msimu ujao wa ligi hiyo maarufu duniani.

Samatta aliyefunga mabao 23 yaliyoisaidia timu yake ya Genk kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya ubeligiji anatajwa kuwa na thamani ya paundi milioni 12 ambayo ni sawa na takribani bilioni 35 za kitanzania,Licha ya kuisaidia timu yake kutwaa ubingwa pia amefanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu ya ubeligiji mwenye asili ya Afrika tuzo ambayo ishawahi kuchukuliwa na wachezaji kama Romelu Lukaku na Vicent Kompany.

Samatta mwenye miaka 26 alijiunga na Genk mwaka 2016 akitokea klabu ya Tp Mazembe ya Kongo huku ikisemekana kuwa timu za Roma ya Italia na Lyon ya nchini Ufaransa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka