Connect with us

Soka

Usajili Yanga Waanikwa

Klabu ya yanga ya jijini Dar es salaam imeripotiwa kukamilisha usajili wa wachezaji kumi mpaka sasa kutoka mataifa tofauti ya Afrika mashariki na Afrika magharibi.Wachezaji hao wanatajwa kuwa ni chaguo la kocha Mwinyi Zahera.

Katika orodha hiyo wapo wachezaji Issa Bigirimana Raia wa Burundi anayeichezea APR ya Rwanda na Patrick Sibomana kutoka Mukura Victory ya nchini humo.Pia wapo Mohamed Camara kutoka Horoya fc na Mburundi Mustafa Suleiman huku Sidney Ukhrob kutoka Namibia na Lamine Moro.

Wachezaji wa ndani waliotajwa kumalizana na Yanga mpaka sasa ni Ally Sonso kutoka Lipuli na Khassim Khamis Abdallah kutoka Kagera sugar Huku Abdulaziz Makame akisajiliwa kutoka Mafunzo na Ally Ally wa Kmc.

Baadhi ya wachezaji walitajwa kumalizana na Yanga lakini inasemekana bado hawajamalizana na klabu hiyo hivyo kutoa nafasi kwa timu nyingine endapo wanajangwani hao watazubaa.Wachezaji kama Metacha Mnata na Vitalis Mayanga imebainika walikua na mazungumzo na klabu hiyo lakini bado hawajasaini mikataba.

Pia imeripotiwa Yanga imechaji Maka Edward amepata timu nchini Latvia hivyo hatokua sehemu ya kikosi cha timu hiyo kwa msimu ujao.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka